image

JALALI TUPE NEEMA, UKUU WAKO UDHIHIRIKE

Likizo kafika, woga kaningia
Moyo umewewesuka,maswali tangia,
Mwana bado kufika,uzito haujaingia,
Jalali tupe Neema, ukuu wako udhihirike

kijasho chembamba katiririka,kamasi kanitoka,
kasakamwa kooni, kakosa kupumua ,
machozi yalengalenga ,ila naficha kwa tabasamu
Jalali tupe Neema, ukuu wako udhihirike.

Moyo wanyauka, maswali nikiyawaza,
Busu natamani, Mola u wapi?
Naomba furaha nirejeshee, jina nipe jipya.
Jalali tupe neema, ukuu wako udhihirike.

Mwaka mpya twaingia ,maswali ni yale yale,
Mungu wetu tusikie ,maana huna likizo,
maombi uyapokee ,wakidhani uko likizo,
Jalali tupe Neema, ukuu wako udhihirike.

Jalali muumba ,kanipa hekima,
Sote hatuwezi toshana, dole gumba na pete,
kiiimo si kimoja, kwa muda mtanisema,
Jalali tupe Neema, ukuu wako udhihirike.

Sala weka mbele,chozi futa mwaya.
Usiwaskize wale,majaliwa watapwaya,
Rabana si mchochole,kakupa hino himaya
Jalali tupe Neema, ukuu wako udhihirike.

©Waiting Wombs Trust